Friday, August 5, 2016

BAYERN KUMUONGEZA MKATABA LEWANDOWSKI.

OFISA mkuu wa Bayern Munich, Karl Heinz-Rummenigge amesema anataka kuongeza mkataba wa Robert Lewandowski lakini ameonya kuwa klabu hiyo haitakuwa tayari kulipa mishahara mkubwa zaidi. Lewandowski mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na Bayern akiwa mchezaji huru akitokea Borussia Dortmund mwaka 2014 na kusaini mkataba utakaomalizika mwaka 2019. Msimu uliopita nahodha huyo wa kimataifa wa Poland alifunga mabao 42 katika mechi 51 alizoichezea Bayern katika mashindano yote na taarifa zilidai Machi mwaka huu kuwa antaka kuongezwa mkataba mpaka mwaka 2021. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo, Rummenigge amesema tayari wameshafanya vikao kadhaa na wakala wake na wako tayari kumuongeza mkataba mwingine. Rummenigge aliendelea kudai kuwa Bayern siku zote imekuwa tayari kuwaongoza mkataba wachezaji wake kabla ya mikataba yao haijamalizika ingawa bado hawajawezi kulipa mishahara mikubw akama wanavyofanya Manchester City na Paris Saint-Germain.

No comments:

Post a Comment