KIUNGO wa Everton, Mohamed Besic anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kufuatia kupata majeruhi ya goti. Nyota huyo wa kimataifa wa Bosnia mwenye umri wa miaka 23 ambaye alijiunga na Everton Julai mwaka 2014, aliumia wakati akicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester United juzi. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Ferencvaros aliichezea Everton mechi 17 katika mshindano yote msimu uliopita. Besic aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akieleza kusikitishwa kwake na majeruhi hayo lakini ameahidi kurejea akiwa imara zaidi.

No comments:
Post a Comment