MATHIEU Debuchy anatarajiwa kujiunga na Galatasaray katika muda wa siku chache zijazo baada ya Arsenal kukubali ofa ya mkopo kwa beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 amecheza mechi 22 pekee toka ajiunge na Arsenal akitokea Newcastle United mwaka 2014 kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara na kupelekea nafasi yake katika kikosi cha kwanza kuchukuliwa na Hector Bellerin. Dubuchy kwasasa yuko na kikosi cha Arsenal kilichopo nchini Norway kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Viking FK na anatarajiwa kufanya uamuzi wa mustakabali wake baada ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya kumalizika. Nusu ya msimu uliopita, Debuchy aliutumia akiwa kwa mkopo katika klabu ya Bordeaux lakini alikosa michuano ya Ulaya baada kuumia wakati wa mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Paris Saint-Germain Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment