BARAZA la uchunguzi la Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limekuta bila hatia ya kuvunja sheria za maadili ya shirikisho hilo, rais Gianni Infantino. Infantino alikuwa akichunguzwa kuona kama kuna uwezekano wa kuvunja sheria yeyote kwa safari alizofanya katika mwezi wake wa kwanza akiwa rais. Lakini baada ya uchunguzi uliochukua wiki kadhaa ambapo mashahidi na Infantino mwenyewe walihojiwa, baraza limeona rais huyo mwenye umri wa miaka 46 hana kesi ya kujibu. Kufuatia uamuzi huo rais na watendaji wengine wa shirikisho hilo wataendelea na shughuli zao kama kawaida kwa ajili ya maendeleo ya soka.
No comments:
Post a Comment