KLABU ya Manchester City chini ya meneja wake mpya Pep Guardiola inakabiliwa na safari ya kwenda Romania kukabiliana na Steaua Bucharest katika mzunguko wa mwisho kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mchezo wa mkondo wa kwanza City watacheza ugenini Agosti 16 mwaka huu kabla ya kurudiana Agosti 24 katika Uwanja wa Etihad. Katika mechi zingine FC Porto ya Ureno wao watapepetana na AS Roma, wakati Villarreal ya Hispania wakicheza AS Monaco ya Ufaransa. Kwingineko Young Boys ya Uswisi wao wanatarajiwa kucheza na Borussia Monchengladbach ya Ujerumani huku Ajax Amstederdam ya Uholanzi wao wakipepetana na Rostov ya Urusi ambao wanshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment