RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ameapa kuwa atakubali hatma yake katika maamuzi yatayotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS juu ya rufani yake kupinga kufungiwa miaka sita kujishughulisha na masuala ya soka. Akihojiwa nje ya ofisi za makahama hiyo huko Lausanne, Uswisi, Blatter mwenye umri wa miaka 80 amesema takubaliana na uamuzi wowote utakaotolewa. Blatter aliongeza kuwa ana matumaini uamuzi utakaotolewa utakuwa mzuri kwa upande wake lakini akiwa kama mwanasoka amejifunza kuwa kuna kushinda na wakati mwingine kushindwa pia. Rais huyo mkongwe alikumbwa na adhabu hiyo kutoka FIFA kufuatia kukutwa na hatia ya kufanya malipo ya dola milioni mbili kwenda kwa rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini mwaka 2011. Mara ya kwanza FIFA ilimlima adhabu ya kumfungia miaka minane Blatter pamoja na Platini lakini adhabu hiyo ilipunguzwa mpaka miaka sita baada ya kukata rufani.
No comments:
Post a Comment