RATIBA ya michuano ya Europa League imepangwa rasmi leo huku klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji anayocheza nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ikipangwa katika kundi F sambamba na timu za Athletic Bilbao na Sassuolo za Hispania na Rapid Vienna ya Australia. Genk walitinga hatua hiyo ya makundi baada ya kuiondosha Lokomotiva Zagreb ya Croatia kwa jumla ya mabao 4-2 huku Samatta akifunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata katika mchezo wa jana. Katika hatua nyingine Manchester United waliopo kundi A wamepangwa kundi moja sambamba na Fenerbahce ya Uturuki, Feyenoord ya Uholanzi na Zorya Luhansk ya Ukraine. Katika mechi za kundi hilo United itakutana na mshambuliaji wake wa zamani Robin van Persie ambaye kwasasa anakipiga Fenerbahce. Mechi za Europa League zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 15 mwaka huu huku mechi za mwisho za makundi zikitarajiwa kuchezwa Desemba 8.
Ratiba kamili ya makundi:
KUNDI A: Man Utd, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya Luhansk
KUNDI B: Olympiacos, Apoel Nicosia, Young Boys, Astana
KUNDI C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
KUNDI D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Tel-Aviv, Dundalk
KUNDI E: Plzen, Roma, Austria Vienna, FC Astra Giurgiu
KUNDI F: Athletic Bilbao, Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
KUNDI G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
KUNDI H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
KUNDI I: Schalke 04, FC Red Bull Salzburg, Krasnodar, Nice
KUNDI J: Fiorentina, PAOK Salonika, Liberec, Qarabag
KUNDI K: Inter Milan, Sparta Prague, Southampton, Hapoel Beer Sheva
KUNDI L: Villarreal, Steaua Bucharest, FC Zurich, Osmanlispor

No comments:
Post a Comment