Saturday, August 27, 2016

LEWANDOWSKI AANZA KWA KISHINDO BUNDESLIGA.



MSHAMBULIAJI nyota wa Bayern Munich, Robert Lewandowski jana ameanza vyema msimu wa Bundesliga kwa kufunga hat-trick wakati wakiilaza Werder Bremen kwa jumla ya mabao 6-0. Mabingwa hao wa Ujerumani walifunga bao la kuongoza kupitia kwa Xabi Alonso kabla ya Lewandowski hajafunga mawili baadae. Nahodha Philipp Lahm na Franck Ribery nao pia walifunga na Lewandowski kuja kufunga bao la tatu kwa penati kufuatia Thiago kufanyiwa madhambi. Thomas Muller yeye alitoa pasi za mwisho tatu kati ya sita zilizozaa mabao hayo katika Uwanja wa Allianz Arena. Beki Mats Hummels ambaye alijiunga na Bayern akitokea Borussia Dortmund kiangazi hiki alicheza dakika zote 90, wakati kiungo chipukizi mwenye umri wa miaka 19 Renato Sanchez aliyenunuliwa kutoka Benfica kwa kitita cha paundi milioni 27.5 hakutumika katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment