NGULI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Arsenal, Thierry Henry anaamini Ubelgiji ina uwezo wa kuweka historia kufuatia kuteuliwa kwake kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Henry atafanya kazi chini ya kocha mkuu Roberto Martinez baada ya kuteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Nguli huyo sasa atafanya kazi na nyota wa Ubelgiji kama Eden Hazard, Kevin De Bruyne na Romelu Lukaku wakati Ubelgiji ikiwa inatafuta nafasi ya kufanikiwa zaidi kuliko ilivyokuwa katika michuano ya Ulaya ambayo walikwamia hatua ya robo fainali. Akihojia Henry amesema kibarua hicho kina changamoto kubwa lakini jambo moja mablo watakwenda kulifanyia kazi ni kuwajengea uwezo wachezaji watambue kuwa wana uwezo wa kuwa timu kubwa. Ubelgiji inatarajiwa kukwaana na Hispania katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Alhamisi hiii kabla ya mechi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cyprus siku tano baadae.
No comments:
Post a Comment