RAIS wa Lyon, Jean-Michel Aulas amesisitiza kuwa Alexandre Lacazette ataendelea kubakia katika klabu hiyo na pia kumtaka Rachid Ghezzal kuongeza mkataba baada ya winga huyo kukaa uhamisho wa kwenda Everton. Mwezi uliopita Lyon ilidai kukataa ofa ya euro milioni 35 za Arsenal kwa ajili ya Lacazette, ingawa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema yuko tayari kuondoka mwezi huu kama klabu itapokea ofa ambayo hawataweza kuikataa. Lacazette ameshafunga mabao matano katika mechi mbili za kwanza za ligi msimu huu na Aulas ameonyesha kuwa na uhakika wa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kubakia hapo mpaka mwishoni mwa msimu huu. Akihojiwa kuhusiana na hilo Aulas amesema Lacazette ni mchezaji muhimu katika kikosi chao hivyo hawana mpango wowote wa kumuachia kiangazi hiki.
No comments:
Post a Comment