KLABU ya Manchester City imekalimisha rasmi usajili wa chipukizi wa kimataifa wa Colombia Marlos Moreno mapema leo. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ametua Etihad akitokea Atletico Nacional na kusaini kataba wa miaka mitano. Hata hivyo, Moreno atapelekwa kwa mkopo katika klabu ya Derpotivo La Coruna na atabakia huko kwa msimu wote wa 2016-2017. Akihojia na mtandao wa klabu hiyo, Moreno amesema City ni klabu kubwa duniani na ni jambo zuri kuwa sehemu ya klabu kubwa kama hiyo.

No comments:
Post a Comment