Saturday, August 6, 2016

SWANSEA YANASA SAINI YA MKONGWE LlORENTE.

KLABU ya Swansea City imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Fernando Llorente kutoka Sevilla jana. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye alikuwa katika kikosi cha Hispania kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2010 na michuano ya Ulaya mwaka 2012, amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Ligi Kuu kwa ada paundi milioni tano. Akihojiwa mara baada ya kukamilisha usajili huo, Llorente amesema amefurahi kujiuanga na Swansea na baada ya kufunga mabao katika Serie A na La Liga sasa anataka kuhamishia makali yake Ligi Kuu. Ujio wa Llorente, hata hivyo unaweza kusukuma kuondoka kwa Andre Ayew kufuatia West Ham United kutajwa kuwa tayari kutoa kitita cha paundi milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana.

No comments:

Post a Comment