MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amesisitiza klabu hiyo inafanya kila wawezalo kuhakikisha wanamsajili Paul Pogba kutoka Juventus kabla ya kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu. Usajili wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa umekuwa ukitawala vyombo vya habari kipindi chote hiki cha kiangazi lakini United wanaonekana kuwa karibu kukamilisha dili hilo la paundi milioni 112 kwa ajili ya kumrejesha tena Old Trafford Pogba. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo kuelekea mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Leicester City, Mourinho amefafanua kuwa dili la Pogba linaweza kukukamilika kabla ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu wa United ambao watacheza dhidi ya Bournemouth Agosti 14 mwaka huu. Mourinho amesema huwa hapendi kuzungumzia wachezaji waliopo klabu zingine na Pogba bado ni mchezaji wa Juventus mpaka hapo itakapothibitishwa rasmi. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa dirisha la usajili linafungwa Agosti 31 mwaka huu na klabu yake inafanya kila wawezalo kukamilisha usajili kabla ya kuanza kwa msimu wa Ligi kuu Agosti 14.

No comments:
Post a Comment