MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta pamoja na klabu yake ya KRC Genk wanakabiliwa na kibarua kimoja cha mwisho kabla ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Europa League. Jana Genk ilifanikiwa kuvuka kikwazo kimoja kwa kuiondosha Cork City FC kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya kushinda mabao 2-1 katika mchezo wao ugenini ambao ulitanguliwa na ule walioshinda bao 1-0 nyumbani. Katika ratiba ya mechi za mwisho za mchujo, Genk sasa wamepangwa kucheza na Lokomotiva Zagreb ya Croatia ambapo kama wakifuzu wataingia moja kwa moja katika hatua makundi ambapo watakutana vigogo mbalimbali wakiwemo Manchester United. Mechi za mkondo wa kwanza za hatua hiyo zinatarajiwa kuchezwa Agosti 18 ambapo timu ya Samatta ya Genk itaanzia ugenini kabla ya kurudiana nyumbani Agosti 25 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment