Monday, August 29, 2016

NASRI AMUWEKA ROHO JUU GUARDIOLA.



KIUNGO wa Manchester City, Samir Nasri amekiri kuwa bado anaweza kuondoka klabuni hapo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kiangazi hiki. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29, alidokezwa kuondoka hapo kufiatia kuwasili kwa Pep Guardiola lakini meneja huyo mpya alimpongeza kiungo huyo baada ya ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya West Ham United jana. Nasri alicheza dakika 15 katika mchezo wa jana ikiwa ni kwanza kwake kwa msimu huu na Guardiola amesema kuwa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal anaweza kubakia City.Akihojiwa kuhusiana na hilo, nasri amesema bado hajajua kama atabakia au ataondoka kiangazi hiki na hilo litategemea a baadhi ya mambo kama yatakaa sawa.

No comments:

Post a Comment