MENEJA wa Valencia, Pako Ayestaran wachezaji wake Shkodran Mustafi na Paco Alcacer hawatauzwa katika kipindi hiki cha usajili wa kiangazi. Mustafi amekuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga na Arsenal wakati Alcacer anekuwa kitajwatajwa kuwindwa na Barcelona. Valencia wanahitaji kuuza wachezaji ili kuepuka kuvunja sheria za matumizi ya fedha, lakini meneja huyo amesisitiza kuwa wachezaji hao hawatakwenda popote kiangazi hiki. Akihojiwa mara baada ya kikosi chake kutandikwa mabao 4-2 nyumbani na Las Palmas jana, Ayestaran amesema Mustafi hatakwenda popote kiangazi hiki.
No comments:
Post a Comment