BEKI wa Paris Saint-Germain-PSG, Serge Aurier amehukumiwa miezi miwili jela kwa tuhuma za kumshambulia ofisa wa polisi. Nyota huyo mwneye umri wa miaka 23 anatuhumiwa kumshambulia polisi huyo baada ya kusimamishwa Mei mwaka huu na kutakiwa kufanyiwa vipimo kama alikuwa na kilevi. Aurier ambaye alikuwa akituhumiwa kumpiga kiwiko kifuani ofisa huyo amedai kuwa aliteswa na polisi na kuna taarifa zinadai kuwa atakata rufani kupinga uamuzi huo wa mahakama. Akihojiwa Juni mwaka huu, Aurier amesema ilikuwa ni vurugu kwani polisi walitoka katika gari lao na kumnyanyapaa, kumtesa na kumpiga usoni. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kinachomsikitisha ni kutuhumiwa kupiga kiwiko polisi kwani kama kweli alitaka kumgusa angeweza kumpiga ngumi usoni. Aurier pia ameamriwa kulipa kiasi cha euro 300 kama fidia kwa majeraha aliyosababisha, euro 300 nyingine kwa uharibifu wa kimaadili na euro 1,500 gharama za kesi.
No comments:
Post a Comment