MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique amemuelezea Lionel Messi kama mfano halisi wa Total Football baada ya kuweka rekodi ya kufunga hat-trick katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Celtic jana usiku. Messi amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi mara sita katika michuano hiyo, wakati Barcelona walipoirarua Celtic kwa mabao 7-0 katika Uwanja wa Camp Nou. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina pia alitengeneza nafasi ya bao la pili la Luis Suarez na pia mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa na Neymar na kuifanya Barcelona kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa mabao 3-0. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Enrique amesema Messi anacheza kokote kwasababu ana uhuru na kutokana na uwezo wake inakuwa sio busara kumbana acheze katika nafasi moja pekee. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Messi ndio mchezaji bora kabisa wa wakati wote kwa mabao na uwezo wake wa soka.
No comments:
Post a Comment