MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simone amekiri Atletico Madrid waliazimika kufanya juhudi kubwa kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya PSV Eindhoven katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika jana. Saul Niguez ndiye aliyefunga bao hilo la pekee katika mchezo huo kwenye dakika ya 43, na kuwafanya Atletico kuanza vyema kampeni zao katika kundi D. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Simeone amesema ulikuwa mchezo mgumu na walifahamu PSV ni timu nzuri na walicheza kama walivyofaya Calderon. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa walipata bao lakini walishindwa kumaliza mchezo kwa nafasi walizopata katika kipindi cha pili iala alama tatu walizopata ni muhimu.
No comments:
Post a Comment