MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema Yaya Toure ataichezea timu hiyo tena pale tu atakapopokea msamaha kwa kauli iliyotolewa na wakal wa mchezaji huyo. Hata hivyo, haiku wazi kama Guardiola anataka msamaha kutoka kwa kiungo huyo au wakala wake. Wakala wa Toure, Dimitri Seluk amedai mteja wake alidhalilishwa kwa nje ya kikosi cha klabu hiyo kinachoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuongeza Guardiola anapaswa kumuomba radhi kama City wakishindwa kutwaa taji hilo. Akiongea na wanahabari mapema leo, Guardiola amesema anapaswa kuwaomba radhi wachezaji wenzake na klabu na kama hatafanya hivyo hatacheza. Wakati huohuo, Toure mwenyewe ametanagza kustaafu soka la kimataifa baada ya kuitumikia Ivory Coast kwa miaka 12. Toure mwenye umri wa miaka 33 ambaye alianza kuitumikia nchi hiyo mwaka 2004, amesema anadhani wakati umefika wa kuacha nafasi kwa vijana wengine wanaochipukia nao kupata nafasi ya kuliwakilisha taifa lao.
No comments:
Post a Comment