MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp ametetea suala la usajili katika kipindi cha nyuma baada ya taarifa kuonyesha kuwa klabu hiyo wamekuwa wauzaji wakubwa katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Taarifa hiyo imegundua kuwa Liverpool wameingiza kiasi cha euro milioni 442 kwa kuuza wachezaji katika kipindi cha miaka sita iliyopita huku Valencia wakishikilia nafasi ya pili kwa kuingiza kiasi cha euro 432 wakifuatiwa na Juventus nafasi ya tatu kwa kuingiza euro milioni 415. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Klopp amesema klabu hiyo kwasasa imebadilika sana na hakuna haja ya kuwa watu wa kuuza wachezaji. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa wanachofanya ni kuimarisha kikosi walichinacho na kuongeza wachezaji wengine kadri itakavyohitajika.
No comments:
Post a Comment