KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez ameanza vibaya kibarua chake hicho baada ya kuchapwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Hispania na kujikuta akizomea na mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo. Martinez raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 43, aliteuliwa kushika nafasi hiyo Agosti 3 mwaka huu ikiwa imepita miezi mitatu toka atimuliwe Everton. Akihojiwa kuhusiana na hilo, Martinez amesema ni jambo lisilowezekana kutegemea mabadiliko makubwa katika kipindi kifupi hivyo mashabiki wanapaswa kuwa na subira. Katika mechi zingine za kirafiki za kimataifa zilizochezwa jana, Ufaransa ilifanikiwa kuichapa Italia mabao 3-1, Ugiriki ikiichapa Uholanzi kwa mabao 2-1 wakati mabingwa wa Ulaya Ureno wakiiburuza Gibraltar kwa mabao 5-0.
No comments:
Post a Comment