Friday, September 2, 2016

MESSI AREJEA KWA KISHINDO ARGENTINA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi amerejea kwa kishindo kulitumikia taifa lake baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Uruguay katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia. Messi alitanagza kustaafu soka la kimataifa baada ya Argentina kupoteza mchezo wa fainali wa michuano ya Copa America dhidi ya Chile kiangazi hiki lakini alibadili uamuzi wake wiki kadhaa baadae. Nyota huyo wa Barcelona alifunga bao hilo katika dakika ya 43 ya mchezo huku Argentina wakimaliza wakiwa pungufu baada ya Paulo Dybala kutolewa kwa kupewa kadi ya pili ya njano. Katika michezo mingine iliyochezwa kwa upande wa Amerika Kusini, Colombia iliitandika Venezuela kwa mabao 2-0, Bolivia ikiichapa Peru kwa mabao 2-0 huku mabingwa wa bara hilo Chile nao wakichapwa na Paraguay kwa mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment