Wednesday, September 7, 2016

MESSI AIPA MATUMAINI BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amerejea mazoezini katika klabu hiyo wakati akikaribia kupona kutoka kwa majeruhi. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alipata majeruhi ya msuli wa paja baada ya kuisaidia nchi yake kuifunga Uruguay hatua ambayo ilimlazimu kuachwa katika mchezo dhidi ya Venezuela. Messi mwenyewe amesisitiza majeruhi yake yanaendelea kupona vyema na kupiga hatua moja kwa kushiriki mazoezi ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo mapema leo. Messi alishiriki sehemu ya kwanza ya mazoezi ambayo yalishirikisha timu yote kabla ya kufanya baadhi ya mazoezi mengine peke yake. Kwa upande mwingine, kiungo Andres Iniesta anatarajiwa kurejea katika mchezo wa La Liga dhidi ya Alaves mwishoni mwa wiki hii baada ya kuka nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja kutokana na majeruhi ya goti.

1 comment: