CHAMA cha Soka cha Qatar kimemtimua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Jose Daniel Carreno raia wa Uruguay ikiwa imepita miezi 17 toka walipomteua kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi. Uamuzi huo umekuja kufuatia timu hiyo kupoteza mechi zake mbili za kufuzu dhidi ya Iran na Ezbekistan. Haijawekwa wazi ni nani haswa ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Carreno lakini kocha mwingine wa Uruguay Jorge Fossati anapewa nafasi kubwa. Kocha mwingine anayepewa nafasi hiyo ni Djamel Belmadi wa Algeria ambaye aliinoa timu hiyo mwaka 2014 hado 2015 wakati Qatar ilipotwaa michuano ya Ubingwa wa Gulf. Kocha mpya atakabiliwa na kibarua kigumu cha kukiandaa kikosi kwa ajili ya mchezo mgumu wa kufuzu dhidi ya Korea Kusini Octoba 6 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment