Thursday, October 6, 2016

CAZORLA KUBAKIA ARSENAL.

KIUNGO wa kimataifa wa Hispania, Santi Cazorla atafurahi akisaini mkataba mpya na Arsenal pamoja na vyombo vya habari vya nchini kwake vikimhusisha na tetesi za kwenda Atletico Madrid. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye aliongeza mkataba wake na Arsenal Julai mwaka jana, amefunga mabao 25 chini ya meneja Arsene Wenger toka amejiunga nao akitokea Malaga mwaka 2012. Akihojiwa Cazorla amesema anafurahia kuwepo Arsenal kwani amekuwa akiaminiwa na Wenger na wachezaji wenzake hivyo anajiona mtu wa umuhimu. Cazorla amefunga mabao mawili katika mechi saba za Ligi Kuu msimu huu, huku Arsenal ikishika nafasi ya tatu katika msimamo.

No comments:

Post a Comment