BEKI wa zamani wa Ligi Kuu Antonio Luna na mchezaji mwenzake wa timu ya Eibar Sergi Enrich wameomba radhi baada ya picha za video wakifanya mapenzi kuvuja mitandaoni. Luna ambaye aliwahi kuchezea Aston Villa na Enrich walijirekodi wenyewe wakifanya mapenzi na mwanamke ambaye jina lake halijajulikana huku wote wakidai ilikuwa ni suala la hiari. Luna na Enrich wameeleza kujutia kitendo hicho cha binafsi kusambaa katika mitandao huku wakijilaumu wenyewe kwa kuvuja huko. Wachezaji hao pia wameomba radhi kwa kushusha heshima ya klabu yao na wao wenyewe na kuongeza kuwa haikuwa nia yao kwa video hiyo kusambaa. Luna alicheza Aston Villa kwa misimu miwili na mkataba wake ulitenguliwa ikiwa imebaki mwaka mmoja na kwenda kujiunga na Eibar kiangazi mwaka jana.
No comments:
Post a Comment