Thursday, October 6, 2016

ORIGI KUKOMAA LIVERPOOL PAMOJA NA KUKOSA NAMBA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool, Divock Origi hana shaka kwa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza msimu huu na anafahamu kuwa nafasi yake ya kuanza itakuja siku zijazo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, ametokea benchi katika mechi tano za Ligi Kuu msimu huu lakini amefunga mabao katika mechi mbili alizoanza ya Kombe la Ligi dhidi ya Burton Albion na Derby Count. Origi amefunga mabao 10 chini ya Jurgen Klopp msimu uliopita yakiwemo matano katika mechi sita za mwisho. Akihojiwa Origi amesema Klopp anamwamini na amewambia kuwa avumilie kwani nafasi yake itakuja.

No comments:

Post a Comment