Thursday, October 6, 2016

DE BRUYNE KUIKOSA BARCELONA.

TAARIFA zinadai kuwa kiungo mahiri wa Manchester City, Kevin De Bruyne hatarajiwi kurejea uwanjani kwa wakati kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona utakaofanyika katika Uwanja wa camp Nou Octoba 19 mwaka huu. Kurejea kwa De Bruyne kunaweza kucheleweshwa ili kuhakikisha amepona kabisa majeruhi ya msuli wa paja aliyopata katika ushindi dhidi ya Swansea City uliofanyika Septemba 24 mwaka huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alikuwa akitegemewa kurejea uwanjani baada ya wiki nne lakini taarifa zilizozagaa zimedai kuwa hataweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo dhidi ya Barcelona. De Bruyne mwenye umri wa miaka 25 alisafiri kwenda jijini Barcel;ona kwa ajili ya matibabu kutoka kwa daktari bingwa Ramon Cugat sambamba na mchezaji mwenzake wa City na Ubelgiji Vincent Kompany ambaye aliumia nyonga.

No comments:

Post a Comment