MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amemtaja nguli wa zamani wa Barcelona na Uholanzi Johan Cruyff kama mtu ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yake. Guardiola amejiimarisha mwenyewe na kuwa mmoja kati ya makocha bora kabisa katika kizazi chake baada ya kushinda mataji kadhaa akiwa na timu za Barcelona na Bayern Munich. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 45, aliwahi kucheza chini ya Cruyff wakati Mholanzi huyo alipokuja kuwa mmoja kati ya makocha bora kabisa wa Barcelona na Guardiola anaamini darasa alilokuwa akimpa wakati huo lilichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yake ya sasa. Akihojiwa Guardiola amesema anajiona mtu mwenye bahati kwani amefundisha City, Bayern na Barcelona kwasababu alikutana naye. Meneja huyo aliendelea kudai alikuwa akidhani anajua soka lakini alipokutana naye dunia mpya ilifunguka mbele yake kutokana na mafundisho yake. Cruyff alifariki kwa saratani ya mapafu Machi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment