Thursday, October 6, 2016

PALERMO KUUZWA KWA WAWEKEZAJI WA CHINA.

RAIS wa Palermo, Maurizio Zamparini anajipanga kuuza sehemu kubwa ya hisa za klabu hiyo kwa kampuni kutoka China ambao atawekeza kiasi cha euro milioni 200 katika timu hiyo. Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 75, ambaye ameshuhudiwa makocha 35 wakibadilishwa toka alipochukua uongozi mwaka 2002, mara ya kwanza kutangaza kuiuza klabu hiyo ya Serie A ilikuwa Machi mwaka huu. Akihojiwa na wanahabari, Zamparini amesema anaiuza Palermo kwa Wachina na wao ndio watakuwa wamiliki wakubwa wa hisa huku yeye akimiliki asilimia kidogo. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa wako katika mazungumzo ya kuwataka wamiliki hao wapya wawekeze euro milioni 200. Zamparini amesema euro milioni 150 zitatumika kwa ajili ya kujenga uwanja wa klabu, euro milioni 30 kwa ajili ya kituo kipya cha mazoezi na euro milioni 20 zilizobakia zitatafutiwa utaratibu mwingine hapo baadae.

No comments:

Post a Comment