RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino amekiri kushangazwa na kusikitishwa na jinsi Sam Allardyce alipojiuzulu nafasi yake ya kuinoa Uingereza baada ya kuitumikia kwa kipindi kifupi. Akihojiwa kushuaiana na suala hilo, Infantino amesema ameshangazwa na pia kusikitishwa na kilichotokea na mambo wanayosoma kuhusiana na sakata hilo. Infantino aliendelea kudai kuwa tukio hilo linasikitisha na sio zuri katika soka lakini anafahamu kuwa Chama cha Soka cha Uingereza-FA kinafuatilia suala hilo na kufanya uchunguzi wao. Allardyce mwenye umri wa miaka 61, alitimuliwa mwezi uliopita baada ya kutoa kauli za fedheha huku akituhumiwa pia kuhusika na suala la umiliki wa tatu wa wachezaji ambalo limepigwa marufuku.
No comments:
Post a Comment