WINGA wa Paris Saint-Germain, Angel Di Maria amedai kuwa kama timu yake ya taifa ya Argentina itapoteza mchezo mwingine wa fainali katika michuano mikubwa atajiuzulu kucheza soka la kimataifa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amekiri kuwa alifikiria kustaafu sambamba na Lionel Messi mapema kiangazi hiki na pia anafikiria kwenda kumuona daktari wa ushauri baada ya kupoteza fainali ya tatu mfululizo. Argentina walipoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani mwaka 2014 kabla ya kufungwa mara mbili na Chile katika fainali za Copa America mwaka 2015 na mwaka huu. Akihojiwa Di Maria amesema ni vigumu sana kupoteza fainali tatu mfululizo ndio maana hata yeye alifikiria kustaafu sambamba na Messi. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kama wakipoteza fainali nyingine siku za usoni ni wazi hataweza tena kuendelea kucheza soka la kimataifa.
No comments:
Post a Comment