MCHEZO wa Clasico ambao Barcelona watakuwa nyumbani kuikaribisha Real Madrid umepangwa kufanyika Desemba 3 mwaka huu. Hatua ya mchezo huo kufanyika siku hiyo utafanya mashabiki wa soka wa Uingereza kushindwa kuuona mchezo huo moja kwa moja katika luninga kutokana na muda uliopangwa. Sheria za Uingereza huwa zinakataza mechi kuonyeshwa moja kwa moja katika luninga nyakati fulani ili kuhamasisha watu wengi waende viwanjani kushuhudia timu zao zikicheza. Msimu uliopita Madrid walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 katika Uwanja wa camp Nou lakini nao walijikuta wakitandikwa mabao 4-0 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Atletico kwasasa ndio wanaongoza La Liga wakifuatiwa na Madrid katika nafasi ya pili na Barcelona wao wanashika nafasi ya nne.
No comments:
Post a Comment