MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amerejea rasmi mazoezini na klabu hiyo leo, wiki tatu baada ya kupata majeruhi ya nyonga. Nyota huyo alipata majeruhi hayo mwezi uliopita katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya bao 1-1. Barcelona ilithibitisha nyota huyo kurejea mazoezini katika kituo chao cha Ciutat Esportiva, ingawa walishindwa kueleza kama atakuwa fiti kwa ajili ya mechi za mashindano. Barcelona inatarajiwa kukutana na Deportivo La Coruna Jumamosi hii huku beki wake Samuel Umtiti naye akirejea mazoezini kufuatia kupona majeruhi ya goti.
No comments:
Post a Comment