KIUNGO mahiri wa Real Madrid, Toni Kroos anatarajia kusaini mkataba mpya mnono na klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani kwasasa ana mkataba na Madrid unaomalizika mwaka 2020 lakini anatarajiwa kuongea mwingine utakaofikia 2022 pamoja na kupandishwa mshahara. Kroos ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wawili wa Madrid waliochezea katika kila mechi msimu huu akiwa sambamba na Alvaro Morata, anadaiwa kuwa atakapokea kitita cha euro milioni 20 kabla ya kukatwa kodi katika mshahara wake mpya. Kwa sasa nyota huyo yuko katika majukumu ya kimataifa na kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani.
No comments:
Post a Comment