WAKALA Mino Raiola amesema atafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kiungo Blaise Matuidi anatoka Paris Saint-Germain na kwenda Juventus kipindi cha majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa akiripotiwa kukaribia kusajili na Juventus majira ya kiangazi lakini mabingwa hao wa Ufaransa walizuia uhamisho wake. Matuidi mwenye umri wa miaka 29, amekuwa akifanya vyema chini ya meneja Unai Emery akiwa ameanza katika kila mchezo hali ambayo inadaiwa itakuwa ngumu kumtoa tena PSG. Hata hivyo, Raiola ameibuka na kudai kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha nyota huyo anakwenda jijini Turin Januari mwakani.
No comments:
Post a Comment