RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino amependekeza kuzikuza fainali za Kombe la Dunia mpaka kufikia timu 48 katika michuano hiyo ikiwa ni idadi kubwa kuliko ile aliyoahidi katika uchaguzi. Infantino raia wa Italia amependekeza timu 16 kati hizo zitaenguliwa baada ya mechi moja ya mtoano na zingine zilizobakia zitaingia katika hatua ya makundi. Sehemu nyingine ya michuano hiyo itabakia kama ilivyo sasa, kwa timu 32 kushindana katika hatua ya makundi baada ya kumaliza hatua ile ya mtoano. Moja ya ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni zake ilikuwa ni kuongeza fainali hizo ili timu zifikie 40. Infantino amesema uamuzi kuhusiana na mapendekezo yake hayo yataamuliwa katika baraza la shirikisho hilo litakalokutana Januari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment