WINGA wa zamani wa Arsenal, Marc Overmars ameunga mkono wazo la Arsene Wenger kwenda kuinoa timu ya taifa ya Uingereza kufuatia kuondoka kwa Sam Allardyce. Uingereza kwasasa haina kocha wa kudumu baada ya Allardyce kuondoka kufuatia kuitumikia timu hiyo kwa siku 67 pekee na nafasi yake kupewa kocha wa muda wa Gareth Southgate. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Overmars amesema Wenger atakuwa ni chagu sahihi kwa Uingereza na anadhani ni wakati wake. Overmars alisajiliwa na Wenger mwaka 1997, na kuja kucheza mechi 142 na kufunga mabao 42 huku akija kuisaidia timu hiyo kutwaa mataji mawili la Ligi Kuu na Kombe la FA msimu wa 1997-1998.
No comments:
Post a Comment