NGULI wa soka wa Cameroon, Rigobert Song mwenye umri wa miaka 40 ambaye yuko katika hali mbaya baada ya kupata kiharusi amezinduka kutoka katika hali ya kutojitambua na kukimbizwa nchini Ufaransa kwa matibabu zaidi. Nahodha huyo wa zamani wan chi hiyo alilazwa katika hospitali jijini Younde, kabla ya kuhamishwa jana jioni kwa ndege maalumu mpaka nchini Ufaransa. Mmoja wa wanafamilia ya nguli amesema Song alisafirishwa akiwa na anajitambua na anapumua mwenyewe bila msaada wa mashine. Song aliugua ghafla juzi wakati akiwa nyumbani kwake na kupoteza fahamu kabla ya kukimbizwa hospitalini.
No comments:
Post a Comment