MSHAMBULIAJI Graziano Pelle ametemwa katika kikosi cha Italia kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Macedonia baada ya kukataa kushikana mkono na kocha Giampiero Ventura kufuatia kutolewa katika dhidi ya Hispania jana. Nyota mwenye umri wa miaka 31 anaykipiga katika klabu za Shandong Luneng, alianza katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 jijini Turin lakini alitolewa nafasi yake kuchukuliwa na Ciro Immobile baada ya kupita saa moja. Hata hivyo mabadiliko hayo yalionyesha kutomfurahisha Pelle na kushindwa kupeana mikono na kocha wake wakati akielekea benchi. Hatua hiyo imechukuliwa kama utovu wa nidhamu na haraka Shirikisho la Soka la Italia-FIGC liliafikiana na kocha wa timu hiyo kumuengua Pelle katika kikosi.
No comments:
Post a Comment