MSHAMBULIAJI nyota wa Ecuador, Enner Valencia mapema leo amefanya kituko cha mwaka kwa kuwakimbia polisi kwa gari la wagonjwa baada ya kudanganya kuumia wakati wa ushindi wa dhidi ya Chile waliopata jana. Nyota huyo ambaye anakipiga Everton kwa mkopo akitokea West Ham United, alivamiwa na polisi wakati akiingia katika Uwanja wa Quito kutokana na tuhuma za kutolipa huduma za mwanae. Baada ya kukwepa kukamatwa katika eneo hilo, Valencia alianza kucheza katika mchezo wa Ecuador kabla ya kujitengenezea mazingira ya kukimbia kwa kubadilishwa na kutoroka kwa gari la wagonjwa huku askari wakimfukuzia kwa mguu. Hata hivyo, vyombo vya habari vya Ecuador vimeripoti kuwa jaji amesitisha kukamatwa kwa Valencia na kumpa muda wa mwisho wa kumaliza mgogoro wake na mke wake wa zamani.
No comments:
Post a Comment