MENEJA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema hatataka kuwa kocha wa Paris Saint-Germain-PSG kwani itakuwa kinyume kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa timu ya nyumbani kwao ya Olympique Marseille. Zidane ambaye aliiongoza Madrid kutwaa taji lao la 11 la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, amesema anafahamu kuwa ipo siku atatimuliwa na klabu hiyo. Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 44, amesema kuinoa Marseille ni jambo ambalo siku moja linaweza kutokea lakini kuifundisha PSG haitawezekana. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kwsasa yuko Madrid na anafurahia kazi yake lakini kamwe hajafikiria sana kuhusu mambo ya mbeleni kwani lolote linaweza kutokea.
No comments:
Post a Comment