Saturday, October 8, 2016

RONALDO AANZA KIBURU BAADA YA KUTUPIA NNE.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amesema amefurahi kuanza tena kuisaidia timu hiyo baada ya kufunga mabao manne katika ushindi wa mabao 6-0 waliopata dhidi ya Andorra jana. Ronaldo aliumia katika mchezo wa fainali ya Ulaya mapema kiangazi na ingawa wachezaji wenzake walikwenda kushinda taji hilo, walipoteza mchezo wao wa ufunguzi wa kufuzu Kombe la Dunia kwa Uswisi mwezi uliopita. Lakini nyota huyo wa Real Madrid amerejea kwa kishindo katika mchezo huo dhidi ya Andorra akifunga mabao mawili katika dakika nne za mwanzo. Akihojiwa Ronaldo amesema walifahamu kuwa bao la kuongoza lilikuwa muhimu kwa timu hiyo ambayo ilikuwa ikijihami sana hivyo amefurahi kufanikisha hilo na kupelekea kupata ushindi mnono. Mabao hayo manne aliyofunga Ronaldo yamemfanya kufikisha mabao 65 katika mechi za kimataifa na anaweza kuongeza mengine zaidi wakati watakapovaana na Visiwa vya Faroe keshokutwa kwenye mchezo mwingine wa kundi B.

No comments:

Post a Comment