Saturday, October 8, 2016

UNICEF YAIPA TANO OLYMPIAKOS KWA KUSAIDIA WATOTO.

SHIRIKA la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa-UNICEF, limebainisha kuwa klabu ya Olympiakos ya Ugiriki imesaidia chanjo kwa watoto zaidi ya 600,000 nchini Chad tokea mwaka 2013. Ushirikiano kati ya klabu hiyo yenye mafanikio katika historia ya soka la Ugiriki na shirika hilo ambalo linahudumia watoto katika nchi zaidi ya 190 duniani, ulianza miaka mitatu iliyopita na toa wakati huo mamia kwa maelfu ya maisha ya watoto yameokolewa. Kampeni ya kinga ya UNICEF hulenga haswa katika nchi ambazo huduma ya chanjo ni duni zikiwemo nchi za Chad, Sudan Kusini na Angola. Msemaji wa UNICEF aliishukuru timu hiyo na wachangiaji wengine wote kwa juhudi zao ambazo zimeokoa watoto 619,582 walio chini ya umri wa mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment