BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Bacary Sagna hana uhakika wa ukubwa wa majeruhi ya msuli wa paja aliyopata katika mchezo wan chi yake dhidi ya Bulgaria, ingawa ana matumaini hayatakuwa makubwa sana. Sagna anatarajiwa kurejea jijini Manchester leo na nafasi yake katika kikosi cha Ufaransa imechukuliwa na beki wa Lille Sebastien Corchia. Beki huyo wa Manchester City ambaye alitolewa katika dakika ya 27 ya mchezo huo wa jana, ana matumaini anaweza kuepuka majeruhi ya muda mrefu. Akihojiwa, Sagna amesema anadhani alichanika kidogo msuli wa paja na anatarajia kufanyiwa vipimo kesho ili kujua ukubwa wa tatizo lake. Katika mchezo huo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia Ufaransa walishinda mabao 4-1 dhidi ya Bulgaria.
No comments:
Post a Comment