KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Kevin-Prince Boateng amemuelezea Ronaldinho kama mmoja kati ya wachezaji bora kabisa aliowahi kucheza nao akiongeza kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ni bora zaidi ya Zinedine Zidane, Diego Maradona na Pele. Kiungo huyo anayekipiga katika klabu za Las Palmas, ambaye aliwahi kucheza na Ronaldinho akiwa AC Milan, amesema mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 alikuwa tayari ameshapita katika ubora wake wakati akisajiliwa na klabu hiyo ya Serie A. Lakini pamoja na umri, Boateng amesisitiza Ronaldinho alikuwa na ubora wa hali ya juu ambao unamtenganisha na nguli wengine katika mchezo huo. Boateng amesema wakati Ronaldinho anatua Milan alikuwa ni tofauti na yule wa zamani lakini pamoja na hayo bado alionesha uwezo wake mkubwa. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa Ronaldinho alikuwa ana uwezo wa kufanya chochote na mpira jambo ambalo linamtenganisha na nguli wengine kama Zidane, Pele na Maradona.
No comments:
Post a Comment