WINGA mahiri wa Leicester City, Riyad Mahrez amebainisha Arsenal ilijaribu kumsajili kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi lakini mabingwa hao wa Ligi Kuu walikataa kumuuza nay eye mwenyewe hakutana kulazimisha kuondoka. Nyota huyo wa kimataifa wa Algeria alikuwa akihusishwa na tetesi za kutua Emirates kwa ajili ya kampeni za 2016-2017, lakini usajili huo hakuwahi kufanikiwa. Akihojiwa Mahrez amesema kulikuwa na mawasiliano na Arsenal lakini Leicester walitaka kumbakisha na walikuwa ghali sana. Nyota huyo aliongeza kuwa hakutaka kuleta mifarakano wakati ofa juu yake ilipotolewa na anadhani alifanya uamuzi sahihi kubakia. Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alisaini mkataba mpya mpaka mwaka 2020, amefunga mabao matatu katika mechi 10 za mashindano yote alizocheza msimu huu.
No comments:
Post a Comment