KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG iko tayari kuongeza juhudi zake za kumsajili nyota wa Barcelona Neymar, na wamepanga kutenga kitita cha euro milioni 200 kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. Baada ya kushindwa kumnasa Cristiano Ronaldo waliyemuwinda kwa kipindi kirefu, viongozi wa klabu hiyo sasa wamehamishia nguvu zao kwa Neymar kuanzia majira ya kiangazi yaliyopita. Mwenyekiti Nasser Al-Khelaifi na ofisa mkuu Olivier Letang walijaribu kumsajili nyota huyo msimu huu kwa kumuahidi mshahara mnono unaofikia ule anaopewa Lionel Messi Barcelona na marupurupu mengine mengi. Hata hivyo, juhudi zao hizo zilikwama kwa neymar kusaini mkataba mpya mwanzoni mwa Julai ambao unamfanya kulipwa kiasi cha euro milioni 25 kwa msimu mpaka mwaka 2021. Pamoja na hayo PSG wanaonyesha kutokana tamaa kwani bado wanataka kumuwania Neymar kwa ahadi ileile ya kumlipa mshahara sawa na Messi ambaye analipwa kiasi cha euro milioni 42 kwa msimu.
No comments:
Post a Comment