BEKI wa kimataifa wa Hispania, Gerard Pique amesema atastaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, kwasababu amechoka jinsi anavyokosolewa na mashabiki. Beki huyo wa Barcelona alikuwa gumzo katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Albania uliochezwa jana baada ya kukata mikono ya fulana yke na kuharibu rangi ya njano na nyekundu kwenye jezi za nchi hiyo. Pique ambaye amekuwa na mahusiano ya mashaka na mashabiki wa Hispania kufuatia mara kadhaa kuzomewa Real Madrid na kuunga kwake mkono kura ya maoni ya kuunga mkono Catalan kujitawala yenyewe, ameshambuliwa vikali katika mitandao ya kijamii kwa hatua yake hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Pique amesema amechoshwa na jinsi anavyoshambuliwa na baada ya Kombe la Dunia nchini Urusi anadhani atakuwa tayari kustaafu soka la kimataifa kwa amani.
No comments:
Post a Comment